Nafasi 32 Za Kazi AFISA TAWALA DARAJA LA II (ADMINISTRATIVE OFFICER GRADE II) 

Nafasi 32 Za Kazi AFISA TAWALA DARAJA LA II (ADMINISTRATIVE OFFICER GRADE II)

MAJUKUMU YA KAZI

  1. Kutoa mapendekezo kuhusu utekelezaji wa Sheria, Sera, Kanuni na Taratibu mbalimbali zinazotolewa na Serikali;
  2. Kutoa mapendekezo kuhusu kazi za utawala na uendeshaji katika Ofisi za Serikali;
  • Kushughulikia masuala ya itifaki mahali pa kazi;
  1. Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu ya Taasisi;
  2. Kupokea na kusajili malalamiko mbalimbali yanayowasilishwa;
  3. Kusimamia miundombinu ya Ofisi na Majengo; Kushiriki katika maandalizi ya Vikao vya Baraza la Wafanyakazi;
  • Kushughulikia masula ya anuai za Jamii;

Kuratibu shughuli za Maafa; na Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na kada yake kama zitakavyoelekezwa na Msimamizi wa kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada katika mojawapo ya fani zifuatazo; Public Administration, Political Science and Public Administration, Business Administration au Commerce iliyojiimarisha katika (Human Resources Management), Leadership and Governance, Public Administration and Management, Local Government and Management, Human Resource Planning and Management, Human Resources Management, Human Resources Planning, Labour Relations and Public Management, Industrial Relations, au fani nyingine zinazoendana na hizo kutoka katika Taasisi au Vyuo vinavyotambulika na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA

TGS.E

MASHARTI YA JUMLA

  1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
  2. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  3. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  4. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
  5. Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma,WASIOMBE na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
  6. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI Computer Certificate

Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

  1. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  2. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  3. Waombaji waliostaafishwa   katika   Utumishi   wa   Umma    hawaruhusiwi   kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  4. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za
  5. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 29 Oktoba, 2025.
  6. Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

KATIBU,

OFISI YA RAIS,

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,

  1. L. P. 2320,

Mtaa wa Mahakama, Tambukareli, DODOMA.

  1. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
  2. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *