Nafasi 3 Za Kazi AFISA UKUZAJI VIUMBE KWENYE MAJI DARAJA LA II (AQUACULTURE OFFICER GRADE II)
MAJUKUMU YA KAZI
- Kutekeleza Sheria na Kanuni zinazohusiana na kuendeleza ukuzaji viumbe kwenye maji;
- Kuhimiza Ukuzaji endelevu wanaokuzwa kwenye maji;
- Kuhamasisha njia bora za uvunaji na uhifadhi wa mazao yatokanayo viumbe wanaokuzwa kwenye maji;
- Kuendesha mafunzo ya ukuzaji viumbe kwenye maji;
- Kusimamia ukusanyaji, uchambuzi na tafsiri ya takwimu za ukuzaji viumbe kwenye maji;
- Kutafiti au kushiriki katika shughuli za utafiti wa ukuzaji viumbe kwenye maji kadri zitakavyojitokeza katika eneo lake la kazi;
- Kukagua ubora wa mazao yatokanayo na ukuzaji viumbe kwenye maji na kuhakikisha yanakidhi viwango vya kitaifa na kimataifa;
- Kuhamasisha kuongeza thamani katika mazao yatokanayo viumbe wanaofugwa kwenye maji, ili kuimarisha biashara na Masoko yake;
- Kukusanya maduhuli yanayotokana na mazao ya Viumbe wanaokuzwa kwenye maji; na
- Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na mkuu wake wa
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye mojawapo ya Shahada ya kwanza katika fani za ukuzaji viumbe kwenye maji (Aquaculture), Sayansi ya kwenye maji na uhifadhi wa mazingira (Aquatic Environmental Sciences and Conservation), Sayansi ya kwenye maji na mazingira (Aquatic Sciences and Environment), Elimu ya viumbe kwenye maji (Marine Biology) kutoka vyuo vyovyote vinavyotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA
TGS.D
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma,WASIOMBE na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI Computer Certificate
Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za
- Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 29 Oktoba, 2025.
- Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
- L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli, DODOMA.
- Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
- Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.