Nafasi 292 AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA II (AGRICULTURAL FIELD OFFICERS)
MAJUKUMU YA KAZI
- Kushirikiana na watafiti kuendesha vishamba vya majaribio,
- Kukusanya/kuhifadhi takwimu za majaribio,
- Kuwafundisha wakulima mbinu za kilimo bora,
- Kuwafikishia wakulima matokeo ya utafiti,
- Kuwafundisha wakulima mbinu bora za kilimo, matumizi ya mbolea na madawa, pembejeo za kilimo,
- Kukusanya na kutunza takwimu za mazao na bei kwa wiki mwezi, robo na mwaka ngazi ya halmashauri,
- Kukusanya takwimu za mvua,
- Kushiriki katika savei za kilimo,
- Kushirikiana na vikundi vya wakulima kuhusu matatizo na teknolojia sahihi za kutumia,
- Kupanga mipango ya uzalishaji,
- Kupima uotaji wa mbegu na kusimamia taratibu za ukaguzi,
- Kutathmini na kusavei maeneo ya vyanzo vya maji kwa ajili ya kuhifadhi,
- Kutunza miti mizazi,
- Kuwatambua wasambazaji wa pembejeo,
- Kutoa mafunzo ya lishe kwa wakulima,
- Kufanya vipimo vya ubora, unyevunyevu na uotaji wa mbegu,
- Kusimamia taratibu za ukaguzi,
- Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea,
- Kusimamia shughuli za kila siku za majaribio ya kilimo,
- Kuwaelimisha wakulima juu ya matumizi bora ya udongo na maji,
- Kutoa ushauri wa kilimo mseto,
- Kuandaa sheria ndogo za hifadhi ya mazingira na
- Kutoa taaluma ya uzalishaji wa mboga, matunda, maua na
SIFA ZA MWOMBAJI
- Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha nne au Sita (VI) wenye stashahada (Diploma) ya kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA
TGS.C
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
- Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma,WASIOMBE na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI Computer Certificate
Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za
- Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 29 Oktoba, 2025.
- Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
- L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli, DODOMA.
- Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
- Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.