Nafasi 131 Za Kazi MHASIBU DARAJA LA II (ACCOUNTANT GRADE II)

Nafasi 131 Za Kazi MHASIBU DARAJA LA II (ACCOUNTANT GRADE II),

MAJUKUMU YA KAZI

  1. Kuandika taarifa ya mapato na matumizi;
  2. Kuandika taarifa za maduhuli;
  • Kupokea maduhuli ya serikali na kupeleka Benki kwa wakati;
  1. Kufanya usuluhisho wa hesabu za Benki na nyingine zinazohusiana na masuala ya fedha;
  2. Kukagua hati za malipo; na
  3. Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na Mkuu wake wa

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Sita wenye shahada ya Uhasibu au Biashara waliojiimarisha kwenye fani ya Uhasibu au Stashahada ya juu ya Uhasibu kutoka Taasisi inayotambuliwa na Serikali pamoja na cheti cha Taaaluma ya Uhasibu CPA(T) au sifa inayolingananayo inayotambuliwa na NBAA.

NGAZI YA MSHAHARA

TGS.D

MASHARTI YA JUMLA

  1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini.
  2. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  3. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  4. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
  5. Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma,WASIOMBE na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
  6. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI Computer Certificate

Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

  1. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  2. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  3. Waombaji waliostaafishwa   katika   Utumishi   wa   Umma    hawaruhusiwi   kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  4. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za
  5. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 29 Oktoba, 2025.
  6. Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;

KATIBU,

OFISI YA RAIS,

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,

  1. L. P. 2320,

Mtaa wa Mahakama, Tambukareli, DODOMA.

  1. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
  2. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *